Hon. Rashid Bedzimba (Kisauni, ODM) Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa na mimi nipenyeze sauti yangu kusema pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia za wanajeshi waliopoteza maisha yao siku ya Alhamisi. Sisi, kama Eneo Bunge la Kisauni, tumempoteza Brigadier Swale Saidi. Alikuwa kijana shupavu mwenye mategemeo yake makubwa...