Hon. Rashid Bedzimba (Kisauni, ODM) Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nichangie Mswada huu. Kwa kweli, nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Barabara zetu nyingi nchini bado hazijakamilika kwa sababu barabara isiyokuwa na nafasi ya watembeaji wa miguu, walemavu, wanaotumia baiskeli za ulemavu na baiskeli, bado haijakamilika....