Hon. Kassim Tandaza (Matuga, ANC) Asante, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza ni kutoa shukrani kwa Mhe. Tim Wanyonyi, gavana mtarajiwa, kwa kuleta Mswada huu muhimu. Nitakuwa mfupi, hasa kwa hili swala linalohusu ardhi kuchukuliwa, na watu na hawawezi kulipwa wakati lishabadilishwa. Nikiwa hapa, najua kwamba kuna ile barabara ya Dongo...