Hon. Haika Mizighi (Taita Taveta County, UDA) Asante sana Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii kuchangia hili swala la maji. Ni kweli maji yamekuwa donda sugu kwa sehemu nyingi za Kenya, haswa katika ile Kaunti yangu ya Taita Taveta. Akina mama, watoto, na wazee wanatembea sehemu mbali sana...