Hon. Harrison Kombe (Magarini, ODM) Asante, Mhe. Spika. Nachukua nafasi hii kumpongeza Mhe. Elsie kwa kuleta Hoja hii. Ni wazi na dhahari kwamba katika shule nyingi, haswa za msingi, watoto wengi hawaendelie na masomo kwa ajili ya janga la njaa. Wakati mwingi utawapata wanahudhuria asubuhi na saa nane hawarudi shuleni...