Hon. Harrison Kombe (Magarini, ODM) Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi niweke sauti yangu kwenye suala hili la usalama nchini. Ningependa kukurudisha nyuma kidogo. Kama utakumbuka, kuna wakati kulikuwa na hali kama hii kule Turkana na Pokot. Tulisafiri, kama Wabunge, na kushiriki katika michezo pamoja na jamii hizo...