Hon. John Paul Mwirigi (Igembe South, UDA) Asante sana Spika wa Muda. Ninaungana na wenzangu kuunga mkono Ripoti hii ya Kamati kwa uteuzi wa wajumbe wa kidiplomasia ambao wanaenda kuwakilisha nchi hii kule nje. Wakati ambapo mabalozi huteuliwa, wao huteuliwa kwa dhana ya nchi, ili nchi iweze kufaidika wakati wanaiwakilisha...