Hon. Paul Katana (Kaloleni, ODM) Asante, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii kuchangia kuhusu ardhi hii. Wakaazi kuhangaishwa na masuala ya mashamba yamezidi sana, hasa sehemu za Pwani. Utakuta watu wamekaa katika mashamba yao kwa muda mrefu sana, lakini kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya maafisa wa Serikali...