Hon. Emmanuel Wangwe (Navakholo, JP) Shukrani sana, Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niulize swali, haswa kwako, kama Spika. Je, mwenzangu, Mbunge wa Kikuyu, anafuata kanuni anapomtaja na kumzungumzia Mheshimiwa Waziri bila Hoja sawasawa, kinyume na Kanuni za Bunge hili? Yale maombi ambayo Mhe. Ichung’wah alikuwa nayo yalikuwa mazuri...