Hon. Onyonka Ahsante, Bw. Spika. Tafadhali, ndugu zangu, muniwie radhi. Tukiikuza lugha yetu ya Kiswahili, Kenya itakuwa nchi nzuri zaidi. Bw. Spika, kwanza, ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu, sisi, kama wanakamati wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, tuliketi pamoja tukakubaliana kuhusu Ripoti hii. Hakuna mwanakamati hata mmoja aliyepinga masuala...