Hon. David Gikaria (Nakuru Town East, UDA) Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ninamshukuru Mhe. Ruweida Mohamed kwa kuwasilisha Mswada huu Bungeni, ambao unalenga kuwajali watu wa maeneo ya Pwani, ambako kuna bahari, na ambapo watu hupoteza maisha au hujeruhiwa kutokana na wanyama walioko baharini. Hili ni jambo muhimu sana kuliangazia....