Hon. Mohammed Ali (Nyali, UDA) Mhe. Spika wa Muda, ninaomba kutoa Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukifahamu kuwa, familia ndiyo kiungo cha msingi cha jamii na kutambua kwamba utamaduni wa Kiafrika unathamini sana asasi ya ndoa ambayo inahakikisha kuendelea kwa binadamu kupitia uzazi; tukizingatia ukweli kwamba, Ibara ya 45 (2) ya Katiba...