Hon. Mpuru Aburi (Tigania East, NOPEU) Mhe. Spika, mimi kwa roho yangu na akili yangu, niko hapa kusema pole kwa Mheshimiwa dada yangu kwa sababu mimi nilikosea kwa kurekodi hiyo video. Ni mimi niliirekodi, kisha baadaye, nikiwa na ndugu na marafiki wetu pale nje, mmoja akaomba “nimsambazie”, kisha nikafanya hivyo....